Thursday, 9 January 2014

Mali asili za Kibindu. Jivunie kwenu.

Mali ya asile si lazima iwe twiga, tembo, dhahabu au almasi. Hata hawa wadudu ni mali yetu ya asili.
Tunapoteketeza misitu na vyanzo vya maji ,wadu hawa wanaopendeza pia wanapotea.

We angalia siku hizi: Ni lini ulimuona CHINGA, KITOFYALA, KASOZI, LWIVI (aina ya KAZILA NJEMO) au KUWI.  Maana hata NGEDA(elegant grasshoper) wanapotea.
Picha za baadhi ya vivutio vya kwetu.
Nilipiga picha hizi Mei , 2013 katika kaeneo tu kadogo nyumbani kwa mama.


 Npumbuzigwe.
 Moja ya aina nyingi za Makunguza






Tuesday, 7 January 2014

Kikao cha Kijiji, Mei 2013. Je matokeo niaje?

Mwaka jana kilifanyika kikao pale Kisatuni kuzungumzia suala la wageni kuvamia hifadhi ya kijiji ,sehemu za Pela hadi mtoni. Wageni hao waliuziwa mashamba au misitu hiyo na baadhi ya viongozi wa kijiji. Lakini kati yao hakukuwa na hata mmoja aliyekuwa na hati miliki ya ardhi. Viongozi wahusika waliingia mtini siku hiyo ya kikao.

Wanakijiji waliwakomalia wageni hao kuwa wavune mazao yao kisha waishie au watafute maeneo halali.
Je suala hili utekelezaji wake umefikia wapi? Wabwanga mbuli ino mwimanya, hegu?!!

Baadi ya picha siku ya kika hicho.


 Masudi Mbalazi akimwaga hoja zake.
 Juma Mgaza aliendesha kikao hicho.


 Mzee Mtiga akitoa hoja yake.


Mmoja wa wageni hao ajijitetea.