Sunday 4 March 2012

Matokeo ya Kidato cha Nne Kibindu. Inasikitisha.

Kwa kweli inabidi wazazi waamke kuhusu suala hili.
Pamoja na mipango mibovu ya serikali ya kuanzisha shule isiyokuwa na walimu wala vifaa, wakazi wa Kibindu inabidi tugangamale ili watoto wetu wapate elimu wanayostahili.
    Wazazi wengi hulipa karo lakini hawafuatilii maendeleo ya vijana wao. walimu wanakula posho bila ya kufanya kazi.

matokeo ya mtihani kibindu

Walimu anazunguuka tu kisatuni na likizo za kila wakati wakati watoto wanabaki tu wakishangaa na kupoteza muda.
Wazazi amkeni,
Pesa ukitoa , basi fuatilia kisomo cha mwana wako.
Washikeni mashati walimu na muwaulize kwanini matokeo yamekuwa kichekesho namna hii.
Darasa zima linaposhidwa kufanya vizuri, basi tatizo sio watoto bali ni mwalimu.
     Suala hili inabidi uongozi wa kijiji ,walimu na wazazi lazima walishughilikie  vinginevyo Kibindu yetu inakuwa kichekesho.

Elimu ni ufunguo wa maisha, kuupoteza ufunguo huo ni sawa na kujitia kitanzi.