Watoto wa shule ya msingi kibindu waliamuliwa kurudi makwao siku chache zilizopita . Sababu ni kwamba wazazi wao wameshindwa kuchangia kununua madawati. Hatua hiyo imechukuliwa ki ubabe tu na mwalimu mkuu bila serikali ya kijiji kujua. Je , hii ni haki? Watoto kuadhibiwa kwa sababu ya wazazi wao kushindwa kutimiza majukumu yao. Hili ni kosa kubwa, na ni kinyume cha tamko la serikali la kutaka kila mtoto apate elimu ya msingi.
Mdau mimi nimekereka saaaana na nitalifuatilia suala hili kwa makini.